International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Novemba 06 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Novemba 06 2024

Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia inataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 32, kabla ya Kombe la Dunia la Klabu msimu ujao. (Mirror)

Barcelona pia wanataka kumsajili Salah mkataba wake wa Liverpool utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Sport - kwa Kihispania)

Liverpool wanapania kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na beki wao wa kimataifa wa Scotland Andy Robertson, 30, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Klabu za Ligi Kuu ya England zimehifadhi haki ya kutafuta fidia kwa mapato yaliyopotea ikiwa Manchester City watapatikana na hatia ya kukiuka kanuni za fedha za ligi. (Times - usajili unahitajika)

Mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Arsenal, Edu alikataa kandarasi mpya ya kusalia na The Gunners ili kuchukua nafasi ya vilabu vingi na mmiliki wa Nottingham Forest Evangelos Marinakis. (Mail)

Manchester United wanapanga kumnunua beki wa Everton na England Jarrad Branthwaite, 22, msimu huu wa joto. (Sportsport)

Mkufunzi mpya wa Manchester United Ruben Amorim anataka wachezaji watatu wa Sporting - beki wa Ureno Goncalo Inacio, 23, mlinzi wa Ivory Coast Ousmane Diomande, 20, na mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26 - kuungana naye Old Trafford. (Sacha Tavolieri, kupitia Teamtalk)

Beki wa England Harry Maguire, 31, hana nia ya kuondoka Manchester United mwezi Januari na anaamini kuwa anaweza kupata kandarasi mpya katika klabu hiyo. (TBR Football)

United itasubiri tathmini ya Bajeti ya Serikali kabla ya kuamua iwapo itabomoa Old Trafford. (Telegraph - usajili unahitajika)

Paris St-Germain wanajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 20, kutoka Aston Villa. (Fichajes - kwa Kihispania) Manchester City wametoa rasilimali kwa ajili ya kusajili wachezaji wawili mwezi Januari baada ya kuanza msimu kwa majeraha. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Chelsea na Uingereza Cole Palmer atafanyiwa uchunguzi wa goti lake la kushoto wiki hii baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuumia katika mechi ya Jumapili dhidi ya Manchester United. (Standard)

Kocha mpya wa England Thomas Tuchel hatashawishi uteuzi wa mkufunzi wa muda Lee Carsley kwa mechi za Ligi ya Mataifa baadaye mwezi huu. (Mail)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
2h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
9h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’