Simba imeendelea kudhihirisha kuwa inautaka ubingwa wa ligi kuu msimu huu wakiichapa KMC mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Simba ilitawala mchezo huo na pengine mambo yangekuwa mabaya zaidi kwa KMC kama washambuliaji wa Simba wangekuwa makini
Awesu Awesu ndiye aliyefungua kalamu ya mabao kwa upande wa Simba akiwaadhibu waajiri wake hao wa zamani
Mabao mengine yalifungwa Jean Charles Ahoua aliyepachika mabao mawili na Edwin Balua
Ahoua sasa amefikisha mabao matano akiwa nyuma wa kinara wa mabao Suleiman Mwalimu kwa tofauti ya bao moja tu
Ahoua amehusika katika mabao 9 ya Simba msimu huu pia akitoka pasi 4 za mabao
Simba imepanda kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 25 na kuishusha Yanga yenye alama 24 katika nafasi ya pili



