Local,Normal News,Singida

Aussems atamba, Singida BS haitanii

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Nov 2024
Aussems atamba, Singida BS haitanii

Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, Patrick Aussems, amesema kikosi chake kitafanya 'maajabu' msimu huu kutokana na aina ya wachezaji alionao

Aussems amesema anaiona timu yake ikifanya vizuri msimu huu na kutoa ushindani kwa klabu kubwa hapa nchini katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea

"Nimekuwa hapa Tanzania kwa miaka kadhaa, naifahamu Ligi Kuu, najua timu kubwa zilizozoeleka ni Simba, Yanga na Azam lakini naiona timu yangu ikiwa kwenye mwelekeo mzuri, tunaweza tukafanya kitu ambacho wengi hawategemei," alisema Aussems

Alisema kikosi chake kina wachezaji wenye uwezo mkubwa, wanaojituma na wanauwezo wa kuipa timu hiyo matokeo mazuri katika mechi zao zijazo

Aliongeza lengo lake ni kuona timu inaendelea kufanya vizuri na kumaliza katika nafasi za juu ili kupata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani

"Hili linawezekana kama tutaendelea kufanya kazi nzuri, wachezaji kujituma na uongozi kufanya kazi yao, hakuna kisichowezekana, naamini tutafanya vizuri," Aussems aliongeza

Singida Black Stars wako katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakikusanya alama 23 kutoka mechi 10. Wamezidiwa alama moja tu na Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 24 huku Simba ikiwa kileleni na alama 25

Hata hivyo Yanga ina mchezo mmoja wa kiporo ambapo leo Alhamisi itacheza dhidi ya Tabora United

IPP Media

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’