Ange Postecoglou anaweza kuwa na kumbukumbu ya wiki zake za kwanza kama meneja wa Tottenham wakati timu yake itamenyana na Galatasaray
Spurs watamenyana na wababe wa Uturuki Super Lig katika Ligi ya Europa Alhamisi usiku na kutakuwa na watu wanaofahamika watakapotinga kwenye Uwanja wa RAMS Park mjini Istanbul
Wachezaji wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza wanaunda washambuliaji wao, nyota wa zamani wa Chelsea, Hakim Ziyech na Michy Batshuayi wakiongoza safu hiyo
Hata hivyo, katika safu ya ulinzi inaundwa na wachezaji wa zamani wa Tottenham Serge Aurier na Davinson Sanchez
Aurier alicheza kaskazini mwa London kutoka 2017 hadi 2021 na licha ya kuwa na wakati mzuri, aliondoka baada ya Postecoglou kutua
Kukutana tena na Sanchez kunaweza kuwa kiwewe zaidi kwa Postecoglou. Mchezaji huyo wa Colombia pia alisajiliwa mwaka 2017, akitokea Ajax, ambapo klabu hiyo hapo awali ilikuwa na mafanikio makubwa katika kuwapata mabeki wa kati wa hali ya juu Jan Vertonghen na Toby Alderweireld
Sanchez alionyesha kuwa tayari kupambana, lakini hakuwahi kuwa katika kiwango cha watangulizi wake, na mnamo 2023 maisha yake na Spurs yalimalizika baada ya Postecoglou kutua
Aurier na Sanchez wanaamini Postecoglou ni sababu ya wao kuondoka Spurs na pengine leo watataka kumthibitishia, alikosea