Yanga hoi mbele ya Tabora United, yapigwa 3-1

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Nov 2024
Yanga hoi mbele ya Tabora United, yapigwa 3-1

Tabora United imewashangaza mabingwa watetezi ligi kuu ya NBC Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Ikitumia mashambulizi ya kushitukiza, Tabora United ikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa Offen Chikola akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Yacouba Songne

Yanga leo ilionekana kuwa na mapungufu makubwa katika safu ya ulinzi pengine kukosekana kwa mabeki wake tegemeo Ibrahim Bacca na Dickson Job kuliigharimu timu hiyo ambapo Miguel Gamondi alilazimika kuwatumia Bakari Nondo Mwamnyeto, Aziz Andambwile ambaye alipata majeraha na Khalid Aucho kurudi kucheza safu ya ulinzi

Wakati wakitafuta mabao ya kusawazisha katika kipindi cha pili, Nelson Munganga alififisha matumaini ya Yanga kifunga bao la tatu katika dakika ya 78

Bao pekee la kufutia machozi lilifungwa na Clemet Mzize kwenye dakika za lala salama

Yanga sasa imepoteza mechi mbili mfululizo wakitoka kupigwa bao 1-0 na Azam Fc hapohapo uwanja wa Azam Complex

Matokeo hayo yameiweka Simba kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 25, huku Yanga ikisalia nafasi ya pili na alama 24

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
36m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’