Prisons kuweka kambi Dar

Joel JJ By Joel JJ β€’ 8th November 2024


Prisons kuweka kambi Dar

Klabu ya Prisons imesema mapumziko ya Kalenda ya Kimataifa kuweka kambi yake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na michezo ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, imeelezwa.

Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha michezo ya kimataifa, huku wachezaji wengi wakitimkia katika vikosi vya timu zao za taifa vinavyosaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), zitakazofanyika mwakani nchini, Morocco

Mtendaji Mkuu wa Prisons, John Matei, amesema kikosi cha timu hiyo kitaanza mazoezi yake rasmi kesho baada ya wachezaji kumaliza mapumziko ya siku sita

Matei alisema baada ya kuifunga KenGold bao 1-0 Jumapili iliyopita, waliamua kuwapa wachezaji wao mapumziko mafupi kwa sababu mechi yao inayofuata dhidi ya JKT Tanzania itachezwa Novemba 24, mwaka huu

"Baada ya kumaliza mechi ya KenGold tulivunja kambi na kuwapa vijana mapumziko ya kama wiki moja au siku sita hivi, Novemba 9 wanatakiwa kurejea kambini kujiandaa na michezo ijayo, kambi yetu kama kila kitu kikienda sawa, tutayafanyia Dar es Salaam, na kipindi chote hiki cha mapumziko ya FIFA, sisi tutakuwa kambini," Matei alisema

Matei alisema sababu kubwa ya kuweka kambi Dar es Salaam ni kuwa karibu na eneo ambalo mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania utachezwa

"Mchezo wetu wa kwanza baada ya mapumziko hayo ni dhidi ya JKT Tanzania uatakaochezwa Dar es Salaam, na hiyo ndiyo sababu kubwa imesababisha tuwe huko karibu zaidi au sehemu hiyo hiyo ambayo tutacheza mchezo wetu wa Novemba 24," Matei aliongeza

Prisons iliyoko chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata, ipo katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 10 kibindoni baada ya kucheza michezo 10, imeshinda miwili, sare nne na kupoteza mechi nne

Kikosi cha JKT Tanzania nacho kinaendelea na mazoezi huku uongozi ukisema wachezaji wote walioumia katika ajali wanaendelea vyema na wameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo

IPP Media


  

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’