Local,Normal News,Simba, Yanga

Simba yatamba baada ya kujikita kileleni

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Nov 2024
Simba yatamba baada ya kujikita kileleni

Kwa sasa furaha imetawala Msimbazi baada ya Simba kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi jana wakijihakikishia kubaki hapo kwa muda mrefu baada ya watani zao Yanga kuangukia pua mbele ya Tabora United wakichapwa mabao 3-1

Matokeo hayo yaliiacha Yanga katika nafasi ya pili ikiwa na alama 24 huku Simba ikibaki kileleni na alama 25 kila timu ikiwa imecheza mechi 10

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali ametamba kuwa msimu huu hakuna wa kuwazuia kutwaa ubingwa wa ligi kuu

Aidha Ahmed amewatahadharisha watani zake Yanga kuwa kama wanataka kuhama dimba la Azam Complex, wasifikirie kabisa kuhamia uwanja wa KMC kwani huko watashuka daraja kabisa

"Nimesikia baada ya kupoteza mechi mbili Azam Complex wanataka kuhama uwanja. Niwatahadharishe wasifikirie kuhamia KMC Complex kwani hii ni himaya yetu sasa"

"Kama wanataka mechi zao zionekane TV 3 basi waje hapa KMC Complex, watacheza ligi ya Championship msimu ujao," alitamba Ahmed

Kumekuwa na tetesi kuwa Yanga inaweza kuhama uwanja wa Azam Complex zikiibuka tuhuma kuwa wanahujumiwa na wamiliki wa uwanja huo Azam Fc

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’