Local,Transfer News,KMC

Kocha KMC anukia Afrika Kusini

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Nov 2024
Kocha KMC anukia Afrika Kusini

TS Galaxy ya Afrika Kusini ambayo Julai mwaka huu ilicheza mechi maalumu ya kirafiki na Yanga ikafungwa 1-0 inadaiwa ipo katika mazungumzo ya kumng'oa kocha wa KMC, Abdihamid Moallin ili akaifundishe timu hiyo

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa KMC zimebainisha kuwa Moallin ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kujiunga nao huku meneja wake akiwa katika mazungumzo hayo na viongozi wa TS Galaxy, ambao wameonyesha nia ya kuihitaji saini yake

Akizungumzia hilo, Moallin alisema kwa sasa malengo yake ni kutengeneza kikosi cha KMC kiweze kuleta ushindani msimu huu na kama kuna mengine yatatokea ataweka wazi juu ya hatima yake, japo mashabiki wake watambue bado yupo na anawapenda

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungula alisema taarifa za kocha wao kuhitajika hazina ukweli bali ni tetesi tu zinazozushwa mitandaoni, huku akiweka wazi viongozi wote bado wana imani na malengo naye ya muda mrefu

Hatua ya Moallin kuhitajika na timu hiyo inajiri baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho Mjerumani, Sead Ramovic kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya, huku kwa sasa kocha msaidizi, Adnan Beganovic akipewa jukumu hilo la kukisimamia

Ramovic amejiuzulu mwenyewe baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo sita ya Ligi ya Afrika Kusini bila ya ushindi ambapo kati yake ametoka sare miwili na kupoteza minne, akiiacha mkiani mwa msimamo ikiwa na pointi mbili tu

Mwanaspoti

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
40m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
19h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’