Baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Tabora United, tetesi ziligubika hatma ya Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi
Uongozi wa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo ulitaka majibu kutoka kwake kwa nini timu imepoteza mechi mbili mfululizo?
Hata hivyo inaonekana Gamondi amepewa nafasi nyingine baada ya leo kuonekana akisimamia mazoezi yaliyofanyika katika Gymkhana
Yanga imerejea mazoezini leo baada ya mapumziko ya siku chache kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Alex Ngai, amesema bado wana imani na Gamondi akiwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi wowote kwani viongozi wa Yanga bado wana ushirikiano na kocha huyo pamoja na benchi lake la ufundi



