Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids ana matumaini makubwa kuwa project aliyopewa ya kuisuka upya Simba itakuwa na manufaa
Baada ya kutofanya vizuri soka la ndani kwa misimu mitatu mfululizo, Rais wa Heshima wa Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' alifanya uwekezaji mkubwa katika usajili uliopita ambapo takribani Bilioni 8 zilitumika kufanya usajili
Fadlu amesema yeye amekuja na falsafa yake ambayo inaendana na aina ya wachezaji alionao ambao wengi umri wao bado ni mdogo
"Nipo kwenye klabu ya Simba ambapo kuna project mpya yenye wachezaji wengi wapya ambao wamefanya vizuri kwenye klabu walizotoka"
"Mimi kama mwalimu nilianza kuweka mbinu zangu ambazo niliamini zitaisaidia hii project kuanzia siku ya kwanza ya Pre Season"
"Kama Kocha mbinu zako zinategemea zaidi wachezaji ulionao, ikitokea ukaona unaweka mbinu fulani na wachezaji inawapa shida unaiweka pembeni na kujaribu mbinu nyingine hivyo ndivyo ambavyo nafanya," alisema Fadlu katika mahojiano na L'VESTIAIRE PODCAST
Fadlu amefanikiwa kuiimarisha Simba katika miezi yake minne ya kwanza akiiweka Simba kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya mechi 10
Aidha chini yake, Simba pia ilitinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho la CAF