Bao la Vivien Corozane limetosha kuihakikishia Simba Queens ushindi wa bo 1-0 dhidi ya Yanga Princess katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake, WPL uliopigwa uwanja wa KMC Complex leo
Huo ni ushindi wa nne mfululizo kwa Simba Queens ambayo imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 12
Kipigo kicho kinawacha Yanga Princess na hali mbaya zaidi kwani wamekosa ushindi katika mechi nne mfululizo
Kabla ya kupoteza mchezo wa leo, Yanga Princess ilitoka sare mechi zote tatu zilizopita



