Zilianza kama tetesi hatimaye leo uongozi wa Yanga umetangaza kuachana na aliyekuwa kocha wake mkuu Miguel Gamondi pamoja na Kocha Msaidizi Moussa Ndaw
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga mapema leo, mikataba ya makocha hao imesitishwa mara moja huku mchakato wa kusaka warithi wao ikianza
Kibarua cha Gamondi kiliingia mashakani baada ya kupoteza mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Azam Fc na Tabora United
Aliyekuwa Kocha wa KMC Abdihamid Moallin anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha msaidizi wa Yanga huku Kheireddine Madoui raia wa Algeria akitarajiwa kuwa kocha mkuu akitokea klabu ya CS COnstantine




