Local,Normal News,Yanga

Kuzishuhudia Yanga, Al Hilal kiingilio 3,000

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Nov 2024
Kuzishuhudia Yanga, Al Hilal kiingilio 3,000

Mapema leo Yanga ilitangaza viingilio vya mchezo wa kwanza hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumanne, Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 10 jioni

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alitaja viingilio hivyo ambapo VIP A ni Tsh 30,000/-, VIP B Tsh 20,000/-, VIP C Tsh 10,000/-, Machungwa na Mzunguuko ni Tsh 3,000/-. Kamwe alisema mauzo ya tiketi yameanza leo kupitia mitandao ya simu

Msemaji huyo wa Yanga amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuipa hamasa timu yao

Kamwe amesema haijawahi kutokea Yanga ikapoteza mechi tatu mfululizo katika mashindano tofauti hivyo hawako tayari kuona wanakosa ushindi katika mchezo dhidi ya Al Hilal

Kuzindua jezi Novemba 20

Katika hatua nyingine, Kamwe amesema Yanga inatarajiwa kuzindua jezi za Ligi ya Mabingwa, Novemba 20, Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani

Kamwe amesema jezi zitaanza kupatikana Makao Makuu ya klabu na maduka ya GSM kwa Tsh 50,000/-

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’