Pamba Jiji mguu sawa kuikabili Simba

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th November 2024

Pamba Jiji mguu sawa kuikabili Simba

Pamba Jiji Fc imetamba kuwa kuwa klabu ya Simba isitarajie mteremko katika mechi itakayowakutanisha ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa Novemba 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini, Mwanza

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Mathias Wandiba, amesema Simba anakwenda Mwanza katika wakati mbaya kwa sababu malengo yao ni kushinda mechi nne zilizobaki za mzunguko wa kwanza

Wandiba amesema Pamba Jiji inawaambia Simba wajiandae kukutana na ushindani kutokana na wao kuhitaji ushindi katika mechi zote zilizobakia za mzunguko wa kwanza ambazo watacheza nyumbani

"Dhamira yetu ni kufanya vizuri katika michezo yetu minne iliyobaki ya mzunguko wa kwanza, michezo miwili tutacheza nyumbani dhidi ya Simba, Ijumaa ijayo na KenGold, Desemba Mosi, hii tumejiwekea mikakati ni lazima tushinde"

"Kwa bahati nzuri moja kati ya michezo hii mwili tunacheza na Simba, wamekuja kwenye wakati mbaya. Unapocheza na timu kama Simba ni lazima wachezaji wawe vizuri kichwani kiakili, huwezi tu kusema tunatumia mfumo huu, sijui nini, ni lazima uwaweke wachezaji wako vizuri kisaikolojia, kwa sababu wanaweza wakaingia wakafanya kitu hicho kikawaondoa kwenye mchezo moja kwa moja," alisema kocha huyo

Aliongeza anaamini katika mchezo huo Pamba Jiji inaweza kupata ushindi wa kwanza nyumbani kutokana na maandalizi na maboresho ambayo wamefanya ndani ya kikosi chao

Pamba Jiji imeshinda mechi moja tu msimu huu ambapo ilikuwa ugenini dhidi ya Fountain Gate, ikiwafunga mabao 3-1, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mkoani, Manyara

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Pamba Jiji iko kwenye nafasi ya 15, ikiwa na pointi nane, baada ya michezo 11, ikishinda mmoja, sare tano na kupoteza michezo mitano

IPP Media

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’