Osimhen njia nyeupe Uingereza

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th November 2024


Osimhen njia nyeupe Uingereza

Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen, ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo Galatasaray anaweza akajiunga na timu yoyote anayohitaji katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani ikiwa itakuwa tayari kulipa Euro 75 milioni

Osimhen mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake wa sasa na Napoli unatarajiwa kumalizika mwaka 2026

Staa huyu anawindwa na timu nyingi ndani na nje ya bara la Ulaya ikiwemo na Galatarasay anayoichezea kwa sasa ambayo ipo tayari kulipa kiasi cha pesa kinachotakiwa ili kumnunua

Hata hivyo, staa huyu anadaiwa kuwa bado anahitaji kucheza soka la kiushindani na kuna uwezekano wa kutua England mwisho wa msimu huu

Klabu ya Chelsea imeonyesha bado inahitaji kumsajili baada ya kushindwa kufanya hivyo katika dirisha lililopita

Akiwa na Galatasaray msimu huu, Osimhen amecheza mechi tisa na kufunga mabao manane.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.