Ligi 1 bila Messi imeshuka thamani - Petit

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th November 2024


Ligi 1 bila Messi imeshuka thamani - Petit

Nyota wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa Emanuel Petit amesema kuondoka kwa Messi nchini Ufaransa ambapo alikuwa anakipiga PSG kumefanya kushuka thamani kwa kwa Ligi 1 tofauti na ilivyopanda kutokana na uwepo wake

Messi aliondoka Ufaransa msimu uliopita akielekea Marekani ambapo alijiunga na klabu ya Inter Miami

Petit anaamini kuondoka kwa Messi kumekuwa na athari kubwa zaidi kuliko nyota wengine kama Neymar na Kylian Mbappe

"Ligue 1 imeshuka thamani sana kibiashara,haina mvuto sokoni mara baada ya Lionel Messi kuondoka"

"Kipindi anajiunga na PSG ligi ilikuwa chini lakini ndani ya muda mfupi Ligi ilipata wafuatiliaji wengi sana na watu wa TV waliuza sana matangazo yao"

"Kwasasa imekuwa tofauti ligi haina mvuto tena kibiashara. Neymar pamoja na Mbappe pia kuondoka kwao kumechangia ila Messi ndio kamaliza kabisa hakuna anaefuatilia tena,wengi wamebase na RSL na MLS,mpaka hizo ligi zimetuzidi sisi," alisema Petit


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.