Local,Normal News,KenGold

Kapilima kuisuka upya KenGold

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Nov 2024
Kapilima kuisuka upya KenGold

Kocha wa KenGold, Omary Kapilima amesema kipindi hiki ambacho Ligi Kuu Bara imesimama, anaendelea na jukumu kubwa la kuhakikisha anatengeneza balansi nzuri ya kikosi hicho, kuanzia eneo la uzuiaji na ushambuliaji ambalo lina changamoto

Kapilima amezungumza hayo wakati kikosi hicho kikiburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi tano baada ya kushinda mchezo mmoja kati ya 11 iliyocheza

Imepoteza michezo minane na sare mbili. Kwa sasa KenGold inajiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Novemba 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya

Kapilima aliongeza, licha ya muda mchache aliokuwa nao ila atahakikisha anapambana kutengeneza eneo lote la ushambuliaji kwani katika michezo mitatu aliyoiongoza timu hiyo, ameona kuna mwelekeo mzuri unaoweza kumpatia matokeo chanya mbeleni

Kocha huyo aliyefundisha na kucheza timu mbalimbali hapa nchini zikiwemo Majimaji, Yanga na Mtibwa Sugar, amejiunga na kikosi hicho Oktoba 22 mwaka huu akichukua nafasi ya Fikiri Elias aliyeamua kuondoka mwenyewe Septemba 17, mwaka huu

Fikiri aliondoka kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo ambapo aliiongoza katika michezo mitatu tu ya Ligi Kuu Bara na kati yake alipoteza yote akianza kufungwa 3-1 dhidi ya Singida Black Stars, Fountain Gate (2-1) kisha KMC (1-0)

Baada ya hapo kikosi hicho kikaongozwa na Jumanne Challe aliyeipandisha timu hiyo Ligi Kuu Bara kutokea Ligi ya Championship na katika michezo yake mitano aliyoiongoza alishinda mmoja akitoa sare mmoja na kupoteza mitatu

Kitendo cha Challe kutokuwa na sifa za kusimamia benchi la ufundi kwa zaidi ya michezo mitano ya Ligi Kuu Bara, ndipo Kapilima akajiunga na timu hiyo na kukiongoza katika mechi tatu akianza na kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Azam FC

Baada ya hapo, timu hiyo ikatoka sare ya mabao 2-2 na Dodoma Jiji, kisha mechi ya mwisho ikachapwa bao 1-0 na Tanzania Prisons

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’