Morocco aahidi ushindi dhidi ya Guinea

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Nov 2024
Morocco aahidi ushindi dhidi ya Guinea

Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Hemed Morocco amesema wanafahamu mchezo dhidi ya Guinea kesho utaamua hatma yao kama wanafuzu kwa michuano ya Afcon 2025 au la

Morocco amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo na wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi

"Tumerejea salama kutoka Ethiopia, tumepata muda mzuri wa recovery na leo tutaendelea na mazoezi yetu ya mwisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa"

"Jambo linalotupa nguvu ni kwamba wachezaji wote wako katika afya njema kimwili na kiakili. Hii ni mechi ya mwisho ya kuamua hatma yetu, niseme tunalijua hilo"

"Tutapambana kadiri ya uwezo wetu ili kuhakikisha tunapata matokeo muhimu tunayohitaji. Niwaambie Watanzania tuko vizuri pengine kuliko wakati mwingine wowote"

"Wachezaji na sisi tunajua umuhimu wa mchezo huu, hatuna presha kwani naamini tutapata matokeo mazuri," alisema Morocco

Morocco amesema Tanzania haijawahi kuwa na njia rahisi katika kufuzu michuano ya Afcon na mara nyingi wanakata tiketi katika mechi ya mwisho

Hivyo ameiandaa timu kwa kuzingatia mahitaji ya mchezo huo kwani anafahamu ni ushindi pekee ambao utawafanya wafuzu

Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 10 jioni na hautakuwa na kiingilio baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk. Samia Suluhu Hassan kutoa ofa kwa mashabiki kushuhudia mchezo huo bure

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
51m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’