Ramovic ameanza kazi Yanga

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th November 2024

Ramovic ameanza kazi Yanga

Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, kikosi cha Yanga kinarejea mazoezini kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumanne, Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Yanga inarudi mazoezini ikiwa na mabadiliko ya benchi la ufundi ambapo itakuwa siku ya kwanza kazini kwa Kocha Mkuu Sead Ramovic pamoja na kocha msaidizi Mustafa Kodro sambamba na Abdihamid Moallin aliyekuwa kocha wa KMC ambaye kapewa majukumu mapya ya Mkurugenzi wa ufundi

Kocha aliyesitishiwa mkataba Miguel Gamondi alisimamia mazoezi ya timu hiyo wiki iliyopita hadi siku ya Alhamisi pale uongozi ulipofikia uamuzi wa kusitisha mkataba wake na kumtangaza Ramovic aliyetua kutoka klabu ya TS Galaxy ya Afrika Kusini

Baada ya kutambulishwa, Ramovic hakuwa na muda wa kupoteza kwani mwishoni mwa wiki alifanya vikao na uongozi pamoja na benchi la ufundi pia akipata nafasi ya kuifahamu Yanga kwa undani ikiwa ni pamoja na kutazama mechi mbalimbali ambazo Yanga imecheza msimu huu

Kocha huyo raia wa Ujerumani atakuwa na wiki moja ya kukiandaa kikosi chake kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumanne, Novemba 26

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’