Msuva aikaribia rekodi ya Ngasa

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th November 2024

Msuva aikaribia rekodi ya Ngasa

Bao alilofunga juzi katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2025 dhidi ya Ethiopia, limemfanya winga Saimon Msuva kufikisha mabao 23 akiwa katika jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Msuva sasa amebakisha mabao mawili kumfikia mfungaji bora wa muda wote katika timu ya Taifa ya Tanzani, Mrisho Ngasa

Unaweza kusema ni suala la muda tu kwa Msuva kuvunja rekodi hiyo kwani bado ana misimu kadhaa mbele kuendelea kuitumikia Stars kama ataendelea kuwa katika ubora wake

Aidha nahodha wa Stars Mbwana Samatta nae hayuko mbali na rekodi hiyo, yeye akiwa amefunga mabao 22

Kesho Jumanne, Novemba 19 Stars itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Guinea katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi

Tanzania inahitaji kushinda mchezo huo ili kukata tiketi ya michuano hiyo itakayofanyika nchini Morocco mwakani

Pengine itakuwa nafasi kwa Msuva na Samatta kuikaribia zaidi rekodi ya Ngasa iliyodumu kwa muda mrefu

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’