Stars yaramba 700M baada ya kufuzu Afcon 2025

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th November 2024


Stars yaramba 700M baada ya kufuzu Afcon 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameizawadia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Sh700 milioni kama pongezi baada ya timu hiyo kufuzu Afcon 2025 itakayofanyika mwakani nchini Morocco

Stars imefuzu kwenye mashindano hayo Kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuitandika Guinea bao 1-0, katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 61

Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia, Waziri wa Utamadini Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amesema zawadi hiyo imetolewa kwa kuthamini kupambana kwao hadi kufuzu, na tayari pesa hizo zimeingizwa kwenye akaunti ya Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo

Pia Stars imepewa mualiko wa kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Februari mwakani

Tanzania ni miongoni mwa timu 24 zilizofuzu kwa michuano hiyo


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.