Klabu ya Simba leo imetambulisha jezi maalum ambazo zitatumika na klabu hiyo katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kuanzia hatua ya makundi (CAF CC)
Kutokana na kanuni za CAF, Simba na Yanga zinalazimika kutumia jezi zenye mdhamini tofauti na Wadhamini wao wakuu ambao ni kampuni za 'ku-bet', M-Bet na SportPesa
CAF inalinda maslahi ya Mdhamini Mkuu Michuano ya Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho, 1xBet ambayo pia ni kampuni ya ku-bet