Manchester United kujitosa kwa Osimhen

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th November 2024


Manchester United kujitosa kwa Osimhen

Manchester United huenda ikamtumia straika wake raia wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, 23, kama sehemu ya mabadilishano ili kuipata huduma ya straika wa Napoli na Nigeria ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo Galatasaray, Victor Osimhen, 25

Osimhen ambaye mkataba wake na Napoli unamalizika 2026, anadaiwa kuwa na shauku ya kutaka kucheza katika Ligi Kuu England baada ya kushindwa kufanikisha hilo katika dirisha lililopita Ulaya kutokana na dili lake la kujiunga na Chelsea kukwama katika dakika za mwisho mwisho

Kwa sasa bado kuna timu nyingi barani Ulaya zinazoonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo kutokana na kiwango ambacho ameendelea kukionyesha tangu kuanza kwa msimu huu akiwa na Galatasaray katika Ligi Kuu Uturuki ambapo amecheza mechi tisa za michuano yote na kufunga mabao nane

Baadhi ya taarifa zinaeleza kwamba Galatasaray pia inafikiria kumpa ofa nono kwa ajili ya kumbakisha ili aendelee kusalia


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.