Local,Transfer News,Yanga

Mshambuliaji Mganda ajifua na Yanga Avic Town

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Nov 2024
Mshambuliaji Mganda ajifua na Yanga Avic Town

Mshambuliaji Fahad Bayo raia wa Uganda amepata nafasi ya kujifua na kikosi cha Yanga ambapo kama benchi la ufundi litaridhika nae, anaweza kusajiliwa na mabingwa hao wa Tanzania Bara, imefahamika

Bayo ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba katika klabu ya MFK Vyskov inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Czech

Bayo aliitumikia MFK Vyskov katika mechi 42 akifunga mabao nane kutoa pasi moja ya bao

Mshambuliaji huyo ambaye pia ameitumikia timu ya Taifa ya Uganda, ana uzoefu mkubwa katika soka la Kimataifa akicheza klabu kadhaa barani Ulaya

Katika timu ya taifa ya Uganda, Bayo amecheza mechi 21 na kuhusika na mabao tisa, akifunga mabao manane (8) na kupiga pasi moja ya mwisho.

Baadhi ya klabu alizowahi kucheza ndani ya nje ya Afrika ni pamoja na MFK Vyskov (Czech), FC Ashdod (Israel), Bnei Sakhnin (Israel), Buildcon FC (Zambia), Vipers (Uganda) na Proline (Uganda)

Yanga imedhamiria kuongeza mshambuliaji katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Disemba 16 2024

Uamuzi huo umewaweka matatani washambuliaji wa kigeni Prince Dube, Kennedy Musonda na Jean Baleke ambao pengine mmoja kati yao anaweza kuondoka dirisha dogo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’