Nitaifikia rekodi ya Ngasa Stars - Msuva

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st November 2024


Nitaifikia rekodi ya Ngasa Stars - Msuva

Baada ya kufunga bao pekee lililoipeleka Tanzania katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), zitakazofanyika mwakani nchini Morocco, na kufikisha idadi ya mabao 24, winga, Simon Msuva, amesema ataifikia rekodi ya kupachika mabao mengi kwa timu ya Taifa

Bao hilo lililofungwa na Msuva juzi lilifanya afikishe mabao 24, moja nyuma ya kinara, Mrisho Ngasa

Akizungumza baada ya mchezo huo, Msuva alisema kwa msaada wa Mungu anaweza akaifikia rekodi ya Ngasa kama atakuwa sehemu ya kikosi cha Stars kitakachoshiriki fainali hizo

"Kwanza namshukuru Mungu kutuwezesha kufuzu AFCON, cha kwanza ilikuwa kufuzu kabla ya kuangalia rekodi binafsi, naamini kwenye fainali zijazo naweza kufikia rekodi ya kaka yangu Ngasa," alisema Msuva

Alisema ushindi walioupata ni kwa ajili ya watanzania wote lakini rasmi anaupeleka kwa walioathirika na ajali ya kuporomoka ya ghorofa yalitokea Kariakoo hapa jijini

"Ushindi huu ni kwa ajili yao, kwa pamoja tunahuzunika na kile kilichotokea kwa wenzetu Kariakoo, natoa pole lakini goli nililofunga nalitoa kwa ajili yao," alisema Msuva

Nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta, anashika nafasi ya tatu akiwa na mabao 22

IPP Media


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.