Local,Normal News,Pamba, Simba

RC Mwanza akanusha kuvamia mazoezi ya Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Nov 2024
RC Mwanza akanusha kuvamia mazoezi ya Simba

Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza imekanusha taarifa zilizosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari zinazodai Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda lea alivamia mazoezi ya Simba yaliyokuwa yakifanyika uwanja wa CCM Kirumba akiwa na askari

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa mkoa kuhusu tukio hilo;

Ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza imesikitishwa na taarifa zilizoenezwa na baadhi ya watu kuwa mkuu wa mkoa Mhe Said Mtanda amevamia mazoezi ya Simba akiwa na polisi na kuwashikili meneja wa timu na kocha msaidizi

Taarifa hizi si sahihi Ukweli ni kuwa mkuu wa mkoa alipokea simu kutoka kwa maafisa wa Jiji la Mwanza kuwa walikuwa wamefungiwa uwanjani CCM kirumba na wanaomba msaada wa Polisi kwenda kuwatoa wakiwa hapo uwanjani kwani walinzi wa Simba waliwazuia kwenye vyumba

Mkuu wa mkoa alimuelekeza kamanda kwenda kuangalia usalama kwenye eneo la tukio lakini na yeye aliamua kwenda kuhakiki ili polisi wasije kuleta taharuki

Alifika kirumba na hakuingia uwanjani alisimama nje ya uwanja na polisi walifanikiwa kuwatoa vijana waliokuwa wamezuiliwa ndani na kwenda kuwahoji, na walifanikiwa kumchukua mlinzi mmoja wa Simba aliyefanya tukio hilo kwa mahojiano aidha kwa tuhuma za kuvunja mlango na vioo vya uwanja

Kama mwenyekiti wa kamati ya usalama anawajibika kusimamia usalama wa wananchi wote wakiwemo hao waliozuiliwa na kufanyiwa shambulio

Hakuna kocha wala kuongozi aliyekamatwa aidha hakuna uvamizi wowote uliofanywa na polisi wala mkuu wa mkoa

Aliyekamatwa alikamatwa baada ya kwisha kwa mazoezi hakukuwa na kuingilia kwa mazoezi ya Simba kwa namna yeyote

Shabiki wa timu yoyote akifanya makosa atachukuliwa hatua za kisheria na polisi wanawajibika kusimamia hilo

Mkuu wa mkoa wa mwanza anawataka wapenzi wa soka kuimarisha amani na usalama katika viwanja vya michezo

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
2h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
6h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
12h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
12h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
12h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
18h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’