Baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili kupisha kalenda ya FIFA, mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inarejea leo ambapo mchezo mmoja utapigwa mkoani Mwanza
Vinara wa ligi hiyo Simba wako ugenini mbele ya Pamba Jiji katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba
Ni mechi inayozikutanisha timu mbili zenye malengo tofauti. Simba inahitaji ushindi ili kuhakikisha inaendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi huku Pamba Jiji wakihitaji ushindi ili kujiondoa katika eneo hatari la kuhuka daraja
Pamba Jiji inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa na alama nane ikiwa imeshinda mechi moja tu na kutoka sare mechi tano na kupoteza mechi tano
Simba inaongoza ligi ikiwa alama 25 baada ya kushinda mechi 8, kutoka sare moja na kupoteza moja
Kumekuwa na mvutano na vita ya maneno baina ya timu hizo nje ya uwanja jambo ambalo linaufanya mchezo huo kuvuta hisia za mashabiki wengi
