Local,Normal News,Azam, Kagera

Toussi apania kuendeleza mwanzo mzuri Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Nov 2024
Toussi apania kuendeleza mwanzo mzuri Azam Fc

Kocha Mkuu wa Azam FC, Rachid Taoussi amesema kikosi hicho kwa sasa kipo tayari kwa ajili ya kuendeleza ushindani msimu huu, wakati itakapocheza na Kagera Sugar Jumamosi hii kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex

Licha ya kukaa wiki mbili bila ya mchezo wowote wa kiushindani, Taoussi ameeleza kuridhishwa na uwezo wa wachezaji katika mazoezi hasa kwa wale waliokosekana timu zao za taifa

"Tumekuwa na maandalizi mazuri na kama nilivyosema tangu awali malengo yetu ni kuendelea kushikilia nafasi tuliyopo na ikiwezekana tuzidi kusogea juu walipo wapinzani wetu, hakuna kilichobadilika zaidi ya morali kwa kila mmoja wao hapa," alisema

Taoussi aliongeza kwamba, jambo zuri ndani ya timu hiyo kwa sasa ni kurejea kwa wachezaji waliokuwa majeruhi akiwemo Sospeter Bajana na Yahya Zayd, ambao wameongeza wigo mpana wa machaguo katika eneo la kiungo cha kati

"Kwa hali ya kikosi kwa sasa ni nzuri na hakuna taarifa ya majeraha mapya ambayo tumeyapata, baada ya ujio wa nyota wengine waliokuwa katika timu za taifa ndipo tutafanya tathimini ya mwisho kwa ajili ya mchezo wetu na Kagera Sugar," alisema Taoussi

Kikosi hicho kitapambana na Kagera Sugar inayojitafuta msimu huu, huku rekodi zikionyesha mara ya mwisho zilipokutana katika Ligi Kuu Bara Uwanja wa Azam Complex, Azam FC ilishinda kwa mabao 5-1

Ilikuwa Mei 25 mwaka huu. Tangu Kocha Taoussi ateuliwe kukiongoza kikosi hicho Septemba 7 mwaka huu akichukua nafasi ya Msenegali, Yousouph Dabo, ameiongoza Azam FC katika michezo tisa ya Ligi Kuu Bara, ameshinda sita, sare miwili na kupoteza mmoja tu

Msimu huu Azam FC imecheza michezo 10 ya Ligi Kuu Bara ikishinda sita, sare mitatu na kupoteza mmoja.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
14h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
17h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
17h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’