Local,Normal News,Yanga

Moallin kuanza na soka la vijana Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Nov 2024
Moallin kuanza na soka la vijana Yanga

Mkurugenzi wa Ufundi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, Abdihamid Moallin, amesema ataifanya timu hiyo kuwa kubwa barani Afrika, lakini pia kuzalisha wachezaji wenye vipaji na 'kulisha' klabu nyingine duniani

Moallin alitangaza kuachana na KMC FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kama Kocha Mkuu na kutua rasmi Jangwani mapema wiki hii

Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kupewa nafasi hiyo, Moallin, alisema lengo lake kubwa ni kuzalisha wachezaji vijana wenye vipaji, kwa sababu yeye ni muumini mkubwa wa kutumia nyota chipukizi

"Lengo ni kuendelea kusaidia kuijenga klabu hii kubwa kwa mwelekeo sahihi, nataka tuwekeze kwa vijana kufanya akademi yetu kuwa moja ya vitalu bora nchini na Afrika kama ilivyokuwa Asec Mimosas ya Ivory Coast"

"Tunataka kuzalisha wachezaji bora kwa ajili ya timu yetu ya kwanza na timu ya Taifa ya Tanzania kwa ujumla, lakini kulisha timu nyingine nje ya nchi ili wacheze mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema Moallin

Bosi huyo mpya alisema mbali na kuzalisha wachezaji kwa ajili ya timu kubwa ya wanaume, lakini pia lengo lake ni kuiimarisha kikosi cha Yanga Princess ili iwe ni timu ya ushindani tofauti na ilivyo sasa

"Tunataka pia kuimarisha pia timu yetu ya wanawake ili nayo ianze kuwania mataji, ili iwe moja ya timu bora Afrika, iliteke soka la Tanzania na kucheza mechi za kimataifa, hasa Ligi ya Mabingwa Afrika ya Wanawake," alisemaΒ 

Aliongeza amekuwa na furaha ya kujiunga na Yanga kwa sababu ametua kwenye klabu kubwa na yenye historia ya kubeba mataji

"Nina furaha sana kuwa Yanga, ni timu kubwa Tanzania na Afrika, naahidi nitashirikiana na wenzangu wa benchi la ufundi ili kuifanya klabu hii iendelee kuwa tishio," Moallin aliongeza

Alilisifia soka la Tanzania limekuwa kwa kasi na kuwafanya wachezaji wengi wa nje ya nchi 'kumiminika' kuja kucheza soka la kulipwa

"Soka la hapa limepiga hatua kubwa sana, kila mtu anaitazama Ligi Kuu ya Tanzania, haishangazi kushika nafasi ya sita Afrika, kiasi imefanya wachezaji wengi wa nje wanatamani kuja kucheza soka nchini, nadhani hili inabidi Watanzania wajivunie," alieleza Moallin

Yanga ilianza kumtangaza Mjerumani, Sead Ramovic, kuchukua mikoba ya Miguel Gamondi na Mustapha Kodro, akiajiriwa kama Kocha Msaidizi, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Msenegal Moussa N'Daw

Kwa sasa Yanga inajiandaa kuikaribisha Al Hilal kutoka Sudan katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa Novemba 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’