International,Normal News,Manchester City

Guardiola ana kazi ya kufanya Manchester City

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Nov 2024
Guardiola ana kazi ya kufanya Manchester City

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amethibitisha kwamba hali ya timu yake ni tete na ikiwa watapoteza mchezo ujao rasmi watakuwa wamelipoteza taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Mabingwa hawa mara nne wa EPL, wikiendi iliyopita waliweka historia ya kupoteza kwa kichapo cha mabao mengi zaidi katika uwanja wao wa nyumbani chini ya Guardiola baada ya kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Tottenham.

Licha ya kichapo hicho, Man City imeendelea kusalia katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 23.

Akizungumzia hali ya kikosi chake, Guardiola alisema wanapitia nyakati ngumu na watahitaji kufanya kitu haraka

"Bila shaka kila kitu hakipo sawa. Katika miaka minane hatujawahi kukutana na hali kama hii. Kwa sasa sisi ni wanyonge. Wakati mwingine unapaswa kupitia hali hii. Unapaswa kukubaliana nayo, huu sio wakati wa kuanza kulaumiana, inatakiwa tukae pamoja na tushikamane, hatupaswi kukimbia," alisema Guardiola.

Kocha huyo pia alisema huu ni wakati ambao wachezaji na timu kwa ujumla inabidi ishikamane zaidi kuliko ilivyowahi kuwa hapo awali na kitu pekee kinachowatofautisha wao ni pale wanapopitia changamoto husimama na kuzikabili kwa pamoja.

Guardiola, ambaye amepoteza mechi tano kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ukocha amesema jambo zuri kwake ni kwamba wachezaji wake huwa wanakosa amani na kuwa na mawazo sana pale wanapopoteza mchezo.

"Kutakuwa na tatizo kama wachezaji wangu hawakuwa na wasiwasi au kama mimi sitakuwa na wasiwasi. Sijui nini kitakachotokea msimu huu, lakini hata kwa sekunde moja sitashindwa kuamini wachezaji. Hakuna timu duniani inayoweza kudumisha mafanikio kwa miaka minane, tisa, kumi mfululizo"

Kocha huyu pia alizungumzia kuhusu mbio za ubingwa akisema ikiwa watapoteza tu mchezo wao wa wiki ijayo dhidi ya Liverpool basi watakuwa wameaga vita ya ubingwa.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’