Local,Normal News,Tabora, Singida

Tabora United yatoshana nguvu na Singida Black Stars

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Nov 2024
Tabora United yatoshana nguvu na Singida Black Stars

Mchezo wa ligi kuu kati ya Tabora United dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora asubuhi ya leo, Jumatatu Novemba 25, umemalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2

Mchezo huo ambao ulipaswa kupigwa jana, uliahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha mkoani Tabora na kujaza maji uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Singida Black Stars watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na alama zote tatu, wakipoteza uongozi wa mabao mawili waliyofunga katika kipindi cha kwanza

Elvis Rupia alitangulia kufunga bao la uongozi kwenye dakika ya 16 kabla ya Anthony Trabi kuongeza bao la pili katika dakika ya 32

Hata hivyo Yacouba Songhne alipunguza mzigo kwa Tabora United kabla ya mapumziko akifunga bao mahiri baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Singida BS pamoja na mlinda lango wao Metacha Mnata

Heritier Makambo aliweka mzani sawa dakika nne baada ya kuanza kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Yacouba aliyeonyesha kiwango bora katika mchezo huo

Matokeo hayo yanaibakisha Singida BS katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 24 sawa na Azam Fc na Yanga ambazo zina uwiano mzuri zaidi wa mabao

Tabora United imesogea hadi nafasi ya tano katika msimamo baada ya kufikisha alama 18

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’