Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Novemba 26 2024

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th November 2024


Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Novemba 26 2024

Meneja mpya wa Manchester United Ruben Amorim anatamani kumsajili winga wa Wolves wa Algeria, Rayan Ait-Nouri, 23. (Sun)

The Red Devils pia wanavutiwa na Christopher Nkunku wa Chelsea lakini wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Borussia Dortmund kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27. (TeamTalks)

Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Bournemouth Mghana Antoine Semenyo, 24, lakini hawana uwezo wa kumnunua mwezi Januari hadi pale wachezaji wengine watakapoondoka .(Sky Sports)

Fulham na Leicester wanatazamia mkataba wa mkopo mwezi Januari kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland, Evan Ferguson, 20. (Football Insider)

Mkufunzi wa Everton Sean Dyche anaungwa mkono kikamilifu na mmiliki wa sasa Farhad Moshiri na ataendelea kuisimamia klabu hiyo siku zijazo. (Sky Sports)

Manchester United wameulizia kuhusu winga wa Sporting U21 mwenye umri wa miaka 17 Geovany Quenda, ambaye thamani yake ni euro 60m (£50.1m). (A Bola – In Portugal)

The Red Devils pia wanalenga idadi ya washambuliaji, huku mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 Randal Kolo Muani wa PSG na mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt wa Misri Omar Marmoush, 25, wakiwa kwenye rada za klabu hiyo. (Sky Germany – In Germany)

United inamfuatilia mshambuliaji wa Wolves na Brazil Matheus Cunha, 25, huku Tottenham pia ikionyesha nia. (TBR Football)

AC Milan wako tayari kushindana na Newcastle kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Everton mwenye umri wa miaka 27 Dominic Calvert-Lewin, wakati Real Madrid wanafikiria kumnunua mlinzi wa Toffees Muingereza Jarrad Branthwaite, 22. (Teamtalk)

Manchester City wana imani kuwa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 24, atamfuata meneja Pep Guardiola kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Give Me Sport)

Barcelona wanatazamia dili la euro 70m (£58.4m) kumnunua mshambuliaji wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 26, Viktor Gyokeres. (Sport - Spanish)

Brighton wanatarajia kumnunua winga wa Cork City wa wachezaji walio chini ya miaka 18 Matthew Murray kwenye majaribio. (Irish Mirror)

Mlinzi wa PSG na Slovakia Milan Skriniar mwenye umri wa miaka 29 yuko tayari kujiunga na Juventus katika dirisha la uhamisho la Januari. (Foot Mercato – In French)

Tottenham huenda wakatafuta kumsajili mlinda lango mwezi Januari baada ya Muitaliano Guglielmo Vicario, 28, kuvunjika kifundo cha mguu na kuhitaji kufanyiwa upasuaji. (Telegraph – Subscription Required)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.