Gamondi kuibukia Singida BS?

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th November 2024

Gamondi kuibukia Singida BS?

Klabu ya Singida Black Stars jana ilitangaza kuwasimamisha makocha wake wawili, Patrick Aussems na msaidizi wake Dennis Kitambi kutokana na matokeo mabaya, huku ikidaiwa kumwania Miguel Gamondi aliyeachana na Yanga hivi karibuni

Baada ya matokeo ya sare ya mabao 2-2 na Tabora United kwenye Uwanja wa Al Hassan Mwinyi, mchezo wa Ligi Kuu Bara, Singida BS ilitangaza kuwasimamisha makocha hao kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo, ambayo imepoteza mchezo mmoja na kutoka sare miwili kati mechi 11 iliyocheza chini ya makocha hao

Wakati Aussems na msaidizi wake wakiwekwa kando kuna taarifa kuwa Gamondi amekuwa akitajwa kuwa anaweza kwenda kurithi mikoba ya Mfaransa huyo aliyeiongoza Singida katika michezo 10 ya Ligi Kuu Bara akiwa ameshinda saba, ametoka sare miwili na kupoteza mmoja tu dhidi ya Yanga

Timu hiyo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 24 sawa na Yanga na Azam, ikiwa imefunga mabao 15 na kuruhusu sita

Gamondi aliondolewa Yanga Novemba 15, 2024, baada ya uongozi wa timu hiyo kusema kuwa hairidhishwa na matokeo ya timu hiyo ambayo ilikuwa haijapata ushindi kwenye mechi mbili mfululizo akiwa aliipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’