Yanga yaanza kwa kipigo makundi CAFCL

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th November 2024


Yanga yaanza kwa kipigo makundi CAFCL

Yanga imeanza vibaya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika ikikubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Adama Colibaly na Yassir Mozamir yametosha kumuhakikishia kocha Florent Ibenga ushindi muhimu ambao umeipeleka Al Hilal kileleni mwa kundi A

Kocha wa Saed Ramovic ana kazi ya kufanya kwani kikosi chake hakikutengeneza nafasi nyingi licha ya Kennedy Musonda kukosa nafasi adimu katika kipindi cha pili mpira wake wa kichwa ukigonga mwamba

Katika mchezo mwingine wa kundi A uliopigwa DR Congo, TP Mazembe imelazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya MC Alger

Al Hilal wanaongoza kundi A wakiwa na alama tatu huku Mazembe na MC Alger zikifuatia na alama moja na Yanga kuburuza mkia

Ni mchezo wa tatu mfululizo Yanga inapoteza katika mashindano yote


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.