Azam Fc kuikabili Singida Black Stars leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th November 2024


Azam Fc kuikabili Singida Black Stars leo

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mchezo mmoja unatarajiwa kupigwa uwanja wa Azam Complex Azam Fc wakiwa wenyeji wa Singida Black Stars

Ni mechi ya kuamua nani anakaa nafasi ya pili kati ya timu hizo ambazo zote zimekusanya alama 24 baada ya kuchez mechi 11

Azam Fc wana uwiano mzuri wa mabao, wanaishikilia nafasi hiyo kwa sasa mbele ya Yanga na Singida BS

Ushindi kwa Azam Fc utawafanya wasogee karibu zaidi ya Simba inayoongoza ligi ikiws na alama 28 lakini hata matokeo ya sare yatawabakisha katika nafasi hiyohiyo

Lakini kama Singida BS watashinda watasogea hadi nafasi ya pili, sare itawasogeza nafasi ya tatu lakini wakipoteza watasailia katika nafasi yao

Singida BS wako chini ya Kaimu Kocha Mkuu Ramadhan Nsanzurwimo aliyechukua mikoba ya Patrick Aussems aliyetimuliwa baada ya kukosa ushindi katika mechi tatu mfululizo

Mtangane huo unatarajiwa kupigwa saa 1 usiku..


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.