Fountain Gate yawasimamisha Barthez, Abalkassim

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th November 2024

Fountain Gate yawasimamisha Barthez, Abalkassim

Kocha wa makipa wa Fountaine Gate, Ally Mustapha 'Barthez' na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Abalkassim Suleiman wamekiri kusimamishwa na klabu hiyo kwa sababu mbalimbali huku Desemba 6 mwaka huu uongozi ukitarajia kukaa kikao cha kuwajadili

Barthez na Abalkassim walisimamishwa siku moja baada ya timu hiyo kufungwa na Pamba Jiji mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Novemba 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara

Mchezaji Abalkassim amethibitisha kupokea barua yenye makosa mawili"

"Ni kweli nipo nje ya timu na nilipokea barua ya kusimamishwa kwa kosa la kuondoka kambini bila ruhusa lakini pia natuhumiwa kuwa nilicheza vibaya kwenye mchezo dhidi ya Pamba ambao nilionyeshwa kadi nyekundu wakidai kuwa nilifanya makusudi," alisema kiungo huyo na kuongeza

"Baada ya wiki mbili kupita niliwapigia viongozi juu ya sakata hilo niliomba kuonana nao ili wanipe barua ya kuachana na timu kutokana na hayo madai, sikupewa na zaidi wamenitaka nikutane nao tena Desemba 6 mwaka huu kwaajili ya kikao cha kunijadili."

Kwa upande wa Bartez alisema hafahamu sababu za kusimamishwa kwake bali anachoweza kusema yupo nje ya timu hiyo kwa muda anaendelea na shughuli nyingine

"Nafikiri watu sahihi wa kuzungumza nao juu ya sababu za mimi kuondoka ndani ya timu ni viongozi, mimi nipo Dar es Salaam kwa sababu nimeondolewa kwenye majukumu yangu sifahamu sababu ni nini," alisema Barthez ambaye aliwahi kuwa kipa wa Simba na Yanga kabla ya kugeukia katika ukocha.

Mwanaspoti

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’