Azam Fc yaichapa Singida BS 2-1

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th November 2024

Azam Fc yaichapa Singida BS 2-1

Azam Fc imezidi kuisogelea Simba kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya leo kuichapa Singida Black Stars mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Alikuwa ni Feisal Salum 'Fei Toto' aliyeitanguliza Azam Fc mapema kipindi cha kwanza akifunga bao lake la tatu msimu huu baada ya kuunganisha krosi ya Iddi Nado

Azam Fc ilitawala mchezo katika kipindi cha kwanza na ilienda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0

Singida BS walizinduka katika kipindi cha pili lakini ni Azam Fc waliokuwa hatari zaidi kupitia mashambulizi yao ya kushitukiza

Jhonier Blanco akawaongezea bao la pili katika dakika ya 57 akimalizia shambulizi la kushitukiza

Bao pekee la kufutia machozi upande wa Singida BS lilifungwa na Elvis Rupia aliyefunga bao lake la tano msimu huu

Ushindi huo umeifanya Azam Fc ifikishe alama 27 katika nafasi ya pili ikiwa nyuma ya vinara Simba kwa tofauti ya alama 1

Singida BS wamesalia katika nafasi ya nne, walima alizeti hao wakicheza mechi ya nne pasipo kupata ushindi

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’