Azam Fc mechi 6, alama 18

Joel JJ By Joel JJ β€’ 30th November 2024


Azam Fc mechi 6, alama 18

Ushindi wa Azam FC wa mabao 2-1 ilioupata juzi dhidi ya Singida Black Stars kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara imeifanya kuondoka na pointi tatu katika michezo sita mfululizo, huku Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rachid Taoussi akisema kwa sasa timu yake ni imara

Tangu ilipolazimishwa suluhu dhidi ya Mashujaa FC kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Septemba 29 mwaka huu, Azam ikaanza kupata ushindi mfululizo hadi kufikia michezo sita kwa kuifunga Namungo bao 1-0, ikaishindilia Prisons mabao 2-0, ikaipa kipigo cha mabao 4-1, KenGold, kabla ya kuichapa Yanga bao 1-0, baada ya hapo ikaifunga Kagera Sugar bao 1-0, kabla ya juzi kushinda mabao 2-1, mechi ikichezwa, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam

Katika michezo hiyo, dhidi ya Namungo, Prisons na Yanga ilicheza ugenini, huku dhidi ya KenGold, Kagera Sugar na Singida Black Stars ikiwa nyumbani

Azam imecheza michezo saba bila kupoteza, ambapo mara ya mwisho ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba, Septemba 26 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, baada ya hapo ikatoka suluhu dhidi ya Mashujaa FC na kuanza kushinda mfululizo

Kocha Mkuu wa Azam, Taoussi, amesema timu yake kwa sasa imeimarika kwa kutosha, lakini pia amewatahadharisha wachezaji wake kuendelea kuwa makini
  


XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.