Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema katika msimu huu Simba inacheza kwa malengo zaidi ya kusaka alama tatu kila mchezo ili kufanikisha mipango mikubwa waliyonayo
Licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos ya Angola katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho (CAF CC), kumekuwa na ukosoaji juu ya kiwango kilichoonyeshwa na Simba katika mchezo huo
Ahmed amesema michuano hiyo inahitaji zaidi matokeo ya ushindi kuliko maonesho
"Sisi Tumefurahia ushindi tulioupata kwa kuiheshimisha nchi, hii ni michuano ya Afrika, tunachohitaji ni kukusanya pointi tatu kwa maana hiyo tumetimiza malengo"
"Mashindano haya hayahitaji mbwembwe. Kuna wengine wanatubeza kuwa tumepata bao la penalti, lakini wakumbuke kuwa hata kufunga kwa penalti nako kunahitaji umahiri na ufundi"
"Ndiyo maana Simba ilipata penalti yake Ahoua akafunga, wenzetu wakapata lakini kipa wetu Moussa Camara akaokoa, hii yote ni kuonesha tuna wachezaji wenye uwezo, ubora na vipaji, siyo kila penalti ikipatikana basi unaweza kufunga," alisema Ahmed
Ushindi huo uliihakikishia Simba kukusanya alama tatu za kwanza kwenye michuano ya CAF CC msimuu ikiongoza kundi A sambamba na CS Constantine ya Algeria
Mchezo unaofuata Disemba 08 Simba itakuwa ugenini Algria kumenyana na CS Constantine