Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imezitoza faini klabu za Simba na Pamba kufuatia matukio yaliyojitokeza kabla ya mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo Novemba 22 2024
Klabu ya Pamba Jiji imetozwa faini ya Tsh Milioni 5 kufuatia kitendo cha maafisa wake kuingilia mazoezi ya Simba siku moja kabla ya mchezo tukio lililotokea uwanja wa CCM Kirumba
Aidha Simba imetozwa faini ya Tsh Milioni 5 kwa kosa la walinzi wake kufanya vurugu wakati wakijaribu kuwatoa nje ya uwanja maafisa hao wa Pamba
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Bodi, Simba imetakiwa kulipa gharama za uharibifu uliofanyika katika ofisi ya Meneja Msaidizi wa uwanja wa CCM Kirumba

