International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Disemba 03 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Disemba 03 2024

Real Madrid imewasiliana na beki wa Ureno Diogo Dalot, 25, na wameambiwa Manchester United itadai pauni milioni 41.5. Hata hivyo, beki wa Liverpool na Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, anasalia kuwa kipaumbele cha mabingwa hao wa Uhispania. (Relevo - kwa Kihispania)

Winga wa Misri Mohamed Salah yuko tayari kusaini kandarasi mpya ya mwaka mmoja katika klabu ya Liverpool lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anazidi kukasirishwa na jinsi klabu hiyo inavyoshughulikia mazungumzo. (Athletic - usajili unahitajika)

Paris St-Germain hawajafanya mazungumzo na Salah licha ya kuhusishwa na winga huyo. (Sky Sports)

West Ham wanamfikiria kocha wa Porto Sergio Conceicao kuchukua nafasi ya Julen Lopetegui, ambaye mustakabali wake kama kocha unakabiliwa na shinikizo kubwa. (Guardian)

Mkufunzi wa Manchester United Ruben Amorim anatazamiwa kufanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya na winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 22, ambaye kandarasi yake inakamilika msimu wa joto. (Telegraph - usajili unahitajika) Bayern Munich wameanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na winga wa Ujerumani Leroy Sane, 28. (Sky Germany)

Leicester City wanafikiria kusitisha mkataba wa mkopo wa msimu mzima wa mshambuliaji wa Crystal Palace Odsonne Edouard mwenye umri wa miaka 26 mwezi Januari. (Football Insider)

Wayne Rooney anapigania kibarua chake kama mkufunzi wa Plymouth Argyle baada ya matokeo mabaya. Mechi zijazo za nyumbani dhidi ya Oxford United na Swansea City zinakadiriwa kuwa muhimu. (Telegraph - usajili unahitajika)

Real Madrid wanapanga kumpa beki wa Uhispania Raul Asencio mkataba mpya wenye masharti bora zaidi. (Fabrizio Romano) Aston Villa italenga beki mpya wa kulia kwenye dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)

Tottenham na Newcastle United wanamfuatilia beki wa Lens wa Uzbekistan Abdukodir Khusanov, 20. (Telegraph - usajili unahitajika)

West Ham wameamua kumpa Vladimir Coufal mkataba mpya badala ya kumuuza beki huyo wa kulia wa Jamhuri ya Czech mwenye umri wa miaka 32. (Football Insider)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
2h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
6h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
12h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
12h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
12h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
18h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’