Kabunda alia na vipigo mfululizo Namungo Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Dec 2024
Kabunda alia na vipigo mfululizo Namungo Fc

Mshambuliaji wa Namungo, Hassan Kabunda amesema hali inayopitia timu hiyo sio shwari kufuatia matokeo mabaya mfululizo ya Ligi

Juzi Namungo Fc imepoteza mchezo wa 9 nyumbani kwa kuchapwa mabao 2-0 na Yanga katika dimba la Majaliwa

Mechi tano za mwisho, Namungo imeshinda moja dhidi ya Pamba Jiji Oktoba 28 kwa bao 1-0 ikipoteza nne mbele ya Yanga 2-0, Mashujaa 1-0, KMC 1-0 na Simba 3-0.

Kabunda amesema ni kama bahati haiko upande wao kwani wana wachezaji wazuri na kocha mzoefu Juma Mgunda

Aliongeza kuwa matokeo hayo yanawapa wakati mgumu wachezaji na kuwakatisha tamaa licha ya kazi kubwa ya Mgunda kuwarudisha mchezoni.

"Tuna michezo 18 migumu iliyopo mbeleni, tunapitia kipindi kigumu sana cha kukosa matokeo tunaamini timu itakuwa sawa kuna muda wachezaji tunakata tamaa lakini kocha anatupa moyo," alisema Kabunda

Namungo iko nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi ikishinda michezo mitatu na kupoteza tisa ikiwa miongoni mwa timu mbili Ligi Kuu zilizopoteza michezo mingi.

Licha ya matokeo hayo lakini timu hiyo imeruhusu mabao 15 wastani wa kufungwa bao moja kila mechi wakiweka kambani mabao matano na washambuliaji wa Namungo wakiwa hawajatikisa nyavu za wapinzani hadi sasa

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
1h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
3h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
4h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
5h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
6h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
8h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
10h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
11h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
12h ago
READ MORE β†’