Klabu ya Pamba Jiji imetuma maombi kwa klabu ya Dodoma Jiji kwa ajili ya kumtaka mshambuliaji Paul Peter, imefahamika
Pamba Jiji imedhamiria kutumia dirisha dogo la usajili kujiimarisha ambapo wameweka kipaumbele katika eneo la safu ya ushambuliaji
Paul Peter amekuwa na msimu mzuri mpaka sasa akiifungia Dodoma Jiji mabao manne katika ligi kuu ya NBC msimu huu
Hata hivyo Dodoma Jiji hawaonekani kuwa na nia ya kumruhusu nyota huyo wa zamani wa Azam Fc ambapo tayari wameanza mazungumzo ya kumuongeza mkataba
Taarifa zaidi imedokeza hata klabu ya KMC ilihitaji huduma ya mshambuliaji huyo lakini Dodoma Jiji hawakuwa tayari kumuachia