Mchezaji wa Everton, mkongwe Ashley Young atakabiliana na mtoto wake wa miaka 18, Tyler kwenye michuano ya Kombe la FA
Everton imepangwa kumenyana na Peterborough United kwenye Raundi ya Tatu ya Kombe la FA, uwanjani Goodison Park, Januari 11 mwakani
Hiyo inamaana staa huyo wa zamani wa Manchester United, Ashley, 39, atakwaana jino kwa jino na mtoto wake, ambaye anacheza kwenye League One akicheza kikosi cha Under-21 cha Petersborough
Na Young amefurahia jambo hilo kupata nafasi ya kucheza dhidi ya mwanaye akiandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwa ndoto imetimia



