Aussems awashukia viongozi Singida BS

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd December 2024

Aussems awashukia viongozi Singida BS

Aliyekuwa kocha wa Singida Black Stars Patrick Aussems amewaaga wanafamilia wa timu hiyo baada ya mkataba wake pamoja na kocha msaidizi kusitishwa ghafla wiki iliyopita

Katika salamu zake za shukrani, Aussems amewashushia lawama viongozi wa Singida BS kuwa wamekosa weledi wa kuiendesha tmu hiyo

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa  kijamii, Aussems ameandika ujumbe huu;

"Hakika maamuzi yaliyofanyika hayakua kwa sababu ya matokeo. Ilikua furaha kufundisha kundi hili la wachezaji. Lakini Ilikua ni kama jinamizi kila siku kufanya kazi na uongozi usiokua na weledi"

"Nilikua nikilalamikia kila siku kuhusu kukosekana kwa uwezo katika uongozi. Msaidizi wangu, Denis Kitambi na mimi binafsi hatujashangazwa na maamuzi yaliyofikiwa, ilikua ni kama ahueni kwetu"

"Hivyo nadhani sasa mmeshaelewa tatizo lilikua wapi. Ningependa kuwashukuru maelfu ya watu kila kona ya nchi kwa miezi mitano iliyopita waliokuja kwangu kunitakia heri, na kupiga na mimi selfie"

"Najiona bado nilikua napendwa sana na mashabiki wa Simba pamoja na watu wengine pia. Nathamini sana wema na ukarimu wenu. Mwisho, kama isemavyo methali ya kifaransa 'Jamais 2, Sans 3'. Kwa maana ya kuwa jambo ambalo limeshatokea mara mbili nyuma upo uwezekano litatokea mara ya tatu siku za mbeleni. Hivyo labda inawezekana tutaonana tena hivi karibuni," aliandika Aussems

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’