Kikosi cha Simba kimeondoka nchini alfajiri ya leo Jumatano kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa raundi ya pili hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya CS Constantine
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Disemba 08, saa 1 usiku
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza safari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali alitamba kuwa wanakenda Algeria wakiwa na dhamira moja tu, kusaka alama tatu katika mchezo huo
Ahmed amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwaombea ili waweze kufika salama na hatimaye kutetea vyema bendera ya Tanzania katika mchezo huo
Simba itasafiri kwa takribani siku mbili kwani imetoka Dar es salaam na kutarajiwa kutua Instabul, Uturuki leo ambapo kesho Alhamisi wataunganisha ndege nyingine kuelekea Algiers
Wakifika Algiers, Simba wataanza safari nyingine kuelekea mji wa Constantine ambapo ni mwendo wa takribani saa 5 kwa basi na saa 1 na dakika 40 kwa ndege