Kocha mpya wa Leicester Ruud van Nistelrooy amesema hakutaka kuondoka Manchester United akiwa na alitamani kubakia, lakini kwa sasa anaweka nguvu katika klabu yake mpya
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mashetani Wekundu alichukua nafasi ya Steve Cooper siku ya Ijumaa, na kusaini mkataba hadi 2027
Hatua hii inakuja baada ya kocha huyo kuiongoza Man United katika michezo minne kama meneja wa muda Old Trafford, kufuatia kufukuzwa kwa Erik ten Hag
Van Nistelrooy, aliyeletwa na Ten Hag kama meneja msaidizi mwezi Julai, alisimamia ushindi mara tatu na sare moja na kuna maneno kuwa alikasirishwa na kuondoka kwake
"Wakati nilipochukua kazi ya muda nilisema niko hapa kusaidia United na ningependa kubaki kuisaidia United, na nilimaanisha hivyo. Kwa hivyo nilisikitishwa sana, na iliniuma ilinibidi kuondoka, nilitamani kubaki kuleta mabadiliko katika klabu yangu ya zamani"
"Lakini nafarijika kuona United ipo chini ya kocha salama kwa sababu pia ninamuelewa meneja mpya. Nilizungumza na Ruben kuhusu hilo, sawa kwake, mazungumzo yalikuwa ya kushukuru, kati ya meneja," alisema
Van Nistelrooy aliiongoza Leicester Jumanne usiku kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham United ukiwa ushindi wake wa kwanza siku mbili tangu alipojiunga na timu hiyo