Local,Normal News,Azam

Fei Toto anaendeleza alipoishia msimu uliopita

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Dec 2024
Fei Toto anaendeleza alipoishia msimu uliopita

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto', anaongoza kwa kufunga na kutoa pasi nyingi za mwisho katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea

Pia nyota huyo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), anaongoza kwa kufunga mabao mengi kwa penalti. Hadi kufikia raundi ya 13 ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezaji huyo ametoa asisti tano na kuwa juu ya orodha ya wachezaji waliotoa pasi za mwisho nyingi ambazo zilizaa mabao

Fei Toto pia anaongoza kwa kufunga mabao mengi ya penalti, akiwa amefanya hivyo mara tatu. Kiungo huyo wa zamani wa Yanga ambaye amefunga mabao manne katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, matatu ameyafunga kwa penalti katika mchezo kati ya timu yake dhidi ya KenGold, uliochezwa, mechi iliyochezwa Oktoba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam wenyeji wakishinda mabao 4-1

Lingine ikiwa ni Novemba 23, mwaka huu, alipofunga bao pekee kwenye Uwanja huo wa Azam ikishinda 1-0 dhidi ya Kagera Sugar

Wachezaji wanaofuatia kwa kufunga mabao mengi ya penalti, Jean Ahoua na Leonel Ateba, ambao wote wamefunga mabao mawili ya penalti kila mmoja na Ogochukwu Morice wa Tabora United ambaye naye amepachika penalti mbili

Ahoua alifunga katika mchezo kati ya timu yake dhidi ya Dodoma Jiji, ikishinda bao 1-0, na dhidi ya KMC, timu yake ikishinda mabao 4-0, Ateba akipachika penalti zake, katika mchezo dhidi ya Coastal Union zikitoka sare mabao 2-2 na dhidi ya Pamba Jiji, likiwa bao pekee kwenye mechi hiyo, huku Ogochukwu akifunga dhidi ya Pamba Jiji timu yake ikishinda bao 1-0 pamoja na Mashujaa, ikishinda pia bao 1-0

Wakati Fei Toto, akiwa na 'asisti' tano, wachezaji Ahoua wa Simba na Salum Kihimbwa wa Fountaina Gate, wana 'asisti' nne kila mmoja

Jumla ya wachezaji saba wanashika nafasi ya tatu kwa kutoa asisti nyingi, kila mmoja akitoa tatu. Wachezaji hao ni Stephane Aziz Ki wa Yanga, Josephat Bada na Ande Koffi wa Singida Black Stars, Yacouba Songne na Heritier Makambo wa Tabora United, Salehe Masudi wa Pamba na Ismail Mgunda wa Mashujaa

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’