Real Madrid ilipokea kichapo cha mabao 2-1 kwenye LaLiga dhidi ya Athletic Bilbao huku Kylian Mbappe akikosa mkwaju wa penalti tena Jumatano usiku
Alex Berenguer aliwaongoza wenyeji dakika ya 53 kabla ya Mbappe - ambaye alishindwa kufunga penalti ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool wiki iliyopita - kupeleka mkwaju wake karibu sana na kipa wa Bilbao Julen Agirrezabala
Jude Bellingham alionekana kuokoa pointi moja kwa Real baada ya kufunga bao kwa mechi ya nne mfululizo ya ligi zikiwa zimesalia dakika 12 kabla ya mechi kumalizika
Lakini makosa ya Federico Valverde dakika mbili baadaye yalimpa Gorka Guruzeta zawadi ya mshindi mbele ya umati wa San Mames
Real Madrid wamepoteza nafasi ya kuiondoa Fc Barcelona kileleni mwa La Liga baada ya kipigo hicho
Barcelona iliichapa Mallorca mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa siku ya Jumanne