Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mchezo mmoja unatarajiwa kupigwa mkoani Kagera
Wenyeji Kagera Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kaitaba saa 1 usiku
Baada ya kukosa ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa ambao wenyeji walirudisha bao dakika za lala salama na kufanya ubao usome 1-1, hii ni mehci nyingine muhimu kwa Kagera Sugar kubeba alama tatu ili kujiondoa katika eneo la hatari kwenye msimamo wa ligi
Hata hivyo wanakutana na Tanzania Prisons ambayo pia inazihitaji alama tatu kujiondoa kwenye hatari pia
Prisons wamekuwa na mwendo wa kusuasua msimu huu wakichapwa mabao 2-1 na Coastal Union katika mchezo uliopita
Wanashika nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 10 huku Kagera Sugar wakishika nafasi ya 15 wakiwa na alama 9
